Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs C.Mwambegele ametembembea na kukagua vituo vya kupigia kura katika Kata ya Mahege ambayo Leo Julai 13,2023 inafanya uchaguzi mdogo wa Udiwani.
Kata ya Mahege iliyopo Jimbo la Uchaguzi la Kibiti inajumla ya vituo vya kupigia kura 13 vyenye wapiga kura 4,352 ambao wanatarajiwa kupiga kura hii leo.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Jaji (Rufaa) Mwambegele amejiridhisha na kushuhudia zoezi la uchaguzi likiendelea salama huku akitoa pongezi kwa Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kibiti Bw. Hemed Magaro kwa maandalizi mazuri katika vituo vyote 13 vya kupigia kura.
"Niwapongeze kwa maandalizi mazuri, ni dhahiri kuwa taarifa imewafikia wananchi kwani wamejitokeza vituoni kupiga kura" Alisema Jaji Mwambegele.
"Nimeshuhudia zoezi la upigaji kura Mahege, vituo vimefunguliwa kwa wakati na wananchi wamejitokeza kwa wingi kutumia haki yako ya kikatiba kuchagua kiongozi wanaemtaka", Alisema Jaji Rufaa Mwambegele.
Jaji wa Rufaa Mwambegele alitembelea Vituo vya Nyambwanda, Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1, Ofisi ya Mtendaji Kata namba 2, Shule ya msingi Hanga, Zahanati ya Hanga, Mahege shule ya msingi, Tomoni milai, Tomoni shule ya msingi, Nyanjati zahanati, na Nyanjati Ofisi ya Mtendaji Kata. Na vituo 2 ambavyo hawakufika ni kituo cha Saudia na Nyakinyo.
Uchaguzi mdogo wa Udiwani kwa Tanzania Bara unafanyika katika Kata 13.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.