VYUMBA 5 VYA MADARASA KUANZA KUTUMIKA JANUARI
Ni katika Shule ya Msingi Kiasi .
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Kibiti Zakayo Mlenduka (DEO-P) ameongoza msafara wa ukaguzi wa vyumba 5 vya madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi kiasi kata ya Msala vyenye thamani ya tsh.110,000,000 kwa fedha za EP4R na mapato ya ndani.
Katika ziara hiyo baada ya ukaguzi na tathmini ya ujenzi kwa ujumla Afisa Elimu MLenduka amerishishwa na hali halisi ya ujenzi unoendelea ambao mpaka sasa upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji. Pia ameisisitiza mafundi na kamati ya ujenzi kuhakikisha kazi inakamilika kwa muda uliokusudiwa .
Aidha Ujenzi vyumba 2 vya madarasa viko katika hatua ya ukamilishwaji,kazi inayoendelea kwa sasa ni blandalin wakati plasta nje na ndani pamoja na jamvi vikiwa vimekamilika.
Vilevile Vyumba 3 na ofisi ya walimu viko hatua ya kuweka sakafu zoezi linalofuata ni kujaza mchanga na kishindilia na kazi inaendelea.
Naye Mhandisi wa Wilaya Kassim Mponda(DE) akiwa shuleni hapo amewaagiza mafundi kuongeza kasi zaidi ya ujenzi kwani vifaa vyote vinavyotakiwa vipo na hakuna sababu ya kuchelewesha ujenzi huo.
Pia mkaguzi wa ndani wa Wilaya Richard Mwalonde (DIA) mara baada ya kuwasili shuleni hapo alikagua namna mapato na matumizi yanavyotumika katika ujenzi huo na kujiridhisha huku akisisitiza fedha zilizotolewa zitimike kama ilivyokusidiwa.
Msafara huo pia uliwahusisha kaimu Afisa mipango Amina Lilanga na Afisa Elimu Maalum ambaye pia ni mlezi wa kata ya Msala.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.