Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimbwini iliyopo Wilayani Kibiti hii leo tarehe 05,03,2025 wameshiriki katika Mdahalo maalumu wenye lengo la kuongeza uwezo hasa kwa Wanafunzi wa kike huku mada kuu ikiwa ni, Je Kuwawezesha Wanawake na Wasichana kumeweza Kuleta matokeo Chanya Kwenye Jamii zetu?
Mdahalo huo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo katika Wilaya ya Kibiti yanatarajiwa kufanyika Siku ya Alhamisi ya Tarehe 06,03,2025 ambapo sherehe hizo zitaanza kwa Matembezi ya Pamoja kuanzia Kituo cha Maliasili kilichopo katika kata ya KIbiti hadi viwanja vya Samora ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani katika Wilaya ya Kibiti ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Hanan Bafagih,wakati wa mchana na kisha Sherehe hizo zitaendelea kuanzia saa Moja Jioni katika ukumbi wa Top Five ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti Bi.Maria Katemana.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.