WASHINDI NYERERE SUPER CUP WAKABIDHIWA ZAWADI.
23/10/2023.
Mkuu wa wilaya ya kibiti Kanali Joseph Kolombo amekabidhi zawadi za washindi na wadau wa Mashindano ya NYERERE SUPER CUP 2023 leo oktoba 23, ambayo yalizinduliwa septemba 24 na kutamatika oktoba 12 katika uwanja wa Samora kwa kushirikisha jumla ya timu 6 za KIBITI FC, BUNGU FC, MTAWANYA FC, MCHUKWI FC, DIMANI FC na JARIBU FC.
Akikabidhi zawadi hizo Mgeni rasmi Kanali Kolombo amewataka washindi wote kutumia mipira waliyopewa kwa kucheza na kujiimarisha kimazoezi tayari kwa mechi yoyote itakayokuja kucheza nao kwa wakati wote.
"Tunataka michezo iimarike mitaani, mashuleni, vijana wapo, sasa mipira hii mkaifanyie kazi mcheze" Alisema Kanali Kolombo.
Katika makabidhiano hayo mshindi wa kwanza kutoka Kibiti FC amejipatia mipira 3 na jezi pisi mbili na mshindi wa pili ni Mtawanya FC.
Vilevile wadau wa maendeleo ya michezo waliopewa zawadi ya jezi pisi moja moja ni Ofisi ya Mkurugenzi Kibiti, Chama cha walimu, Chama cha corefa kusini, Chuo cha walimu Vikindu na jezi za Marefa kutoka Kibiti Sekondari.
Hata hivyo Kanali Kolombo amekabidhi zawadi za mpira mmoja mmoja kwa shule ya sekondari Zimbwini, Ofisi ya Mganga Mkuu (W) Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (W ), Kikosi cha 830 JKT, Ofisi ya Mkuu wa Polisi Kibiti ( OCD), Ofisi ya Maliasili, Zawadi day care , Sisa hardware na SNKD Investment.
Aidha Kanali Kolombo ameishukuru Taasisi hiyo kwa namna inavyojitoa kuifikia jamii moja kwa moja kwani ni dhana ambayo haitatoka kwenye fikra za wananchi hususani vizazi vinavyoendelea kukua.
Awali timu zote hizo zilipatiwa Vifaa vya maandalizi jezi pisi moja moja na mpira mmoja mmoja kwa ajili ya maandalizi kabla ya kuanza kwa Mashindano hayo.
Kwa upande wa Katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ndugu Omary Abdull Punzi alisema kuwa malengo ya Mashindano yalikuwa kuenzi FIKRA za waasisi wetu na kutoa Elimu ya umuhimu wa Ulinzi Shirikishi na kujiepusha na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya nchini.
Nao baadhi ya wadau waliopati wazawadi wanesema, wamefurahi sana na kupitia Mashindano hayo, watahamadisha na wadau wengine kushiriki michezo mbalimbali kwa maendeleo ya michezo Kibiti.
Mashindano hayo yamesimamiwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya KIBITI sambamba na Wadau waliofanikisha upatikanaji wa zawadi ka vile NSSF, NBC BANK,WCF, TANGANYIKA ORGANIC EMPIRE na ST DAVID COLLEGE OF HEALTH SCIENCES KIMARA TEMBONI, MONICA Foundation,Sadik Mchama na Chama Cha MPIRA mkoa wa Pwani kanda ya Kusini (COREFA).
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.