Ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Mahege utakaofanyika tarehe 13 Julai, 2023, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kibiti Bw. Msena Bina akimwakilisha Msimamizi wa uchaguzi Bw. Hemed Magaro amefungua mafunzo Kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaididizi kwa vituo vya kupigia kura leo tarehe 10 Julai, 2023 katika Shule ya Sekondari Mahege.
Akifungua mafunzo hayo Bw.Bina aliwataka wasimamizi wote kusikiliza kwa makini maelekezo wanayopewa Ili waweze kuelewa namna ya kufanya kazi kwa kuzingatia MAADILI kama ilivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Vilevile Bw. Bina aliwasisitiza wasimamizi wote kuuliza maswali pale wanapoona hawajaelewa ili kupata uelewa utakaowasaidia kufanya kazi kwa ufanisi katika siku ya uchaguzi.
Hata hivyo Wasimamizi Wasaidizi wa Jimbo la Kibiti Bw. Sudi Kassim, waliwapitisha wasimamizi hao kupitia mambo mbalimbali yanayotakiwa kufanyika na kuzingatia wakati wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na wajibu,majukumu na taratibu za uchaguzi.
Awali Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Bungu Mhe. Ally Mohamed Mtile aliwaongoza wasimamizi hao kula kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza Siri za uchaguzi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.