Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Kibiti Bi.Hanan Bafagih leo 23 Novemba Amefungua rasmi mafunzo ya wasimamizi na makarani wa vituo vya Kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya wavulana Kibiti, Bi.Hanan Bafagih amewataka Wasimamizi wa Vituo na Mkarani kuzingatia mafunzo hayo ambayo yameendeshwa na wawezeshaji tofauti tofauti kwa ajili ya kupata uelewa mpana utakaowajengea uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Bi.Hanan ameongeza kwa kuwakumbusha swala la muda hasa muda wa kufungua vituo vya kupigia kura ili kuwawezesha wananchi kutimiza zoezi hilo mapema.
Katika Ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku moja yenye lengo la kuwapatia uwezo wa kufanya kazi wasimamizi wa vituo pamoja na makarani Mkuu wa Wilaya ya Kibiti ambaye alihudhuria ufunguzi huo amewataka wasimamizi pamoja na makarani wateule kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kama ilivyokusudiwa.
‘’Ninyi mmeaminiwa na kupata nafasi hii ya kufanya kazi kwa sababu mmeonekana mnastahili na kila mtu ambae amechaguliwa ana wajibu katika hili,hakuna alieteuliwa kwa bahati mbaya
Aidha Kanali Kolombo amewataka wasimamizi hao wa vituo Pamoja na makarani kuwa wazalendo katika kazi na kuzingatia kanuni sheria na taratibu ili kutimiza kwa usahihi wajibu wao.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.