Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imekuwa ikiendelea na mapambano dhidi ya utapiamlo lengo likiwa ni kuifikia jamii na kutokomeza kabisa utapiamlo wa aina zote nchini ili kuhakikisha kunakuwa na kizazi chenye siha njema.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele ambaye alikua akishuhudia kusainiwa kwa mkataba wa lishe baina ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti na watendaji wa kata katika kikao cha tathmini kilichofanyika kwenywe ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa wilaya ya kibiti.
Katika mkutano huo Meja Gowele amewaagiza watendaji wa Kata kupitia mkataba huo waliosaini kuhakikisha lishe ni ajenda ya kudumu katika vikao vya kisheria vya kamati ya maendeleo ya kata.
Vilevile Gowele amesema kuwa,lishe bora katika jamii ndiyo kichocheo muhimu katika maendeleo ya jamii kwa ujumla hivyo ikiwa lishe ni duni athari za Utapiamlo zitakua kubwa hususani kwa kina mama wajawazito na Watoto wenye umri chini ya miaka.
Aidha Gowele amewataka viongozi wa wilaya kuendelea kutoa elimu ya lishe sambamba na kuongeza uhamasishaji katika maeneo ya kilimo na mifugo ili kupata uzalishaji wa vyakula vyenye virutubishi na kuwa na uhakika wa vyakula katika kaya mbalimbali.
Naye Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Dr Elizabeth Oming’o alisema ‘kwa upande wa wazalishaji wa chumvi katika maeneo ya delta,vijijini na kwingineko ambako huzalisha chumvi kwa wingi amesema,wataendelea na wanaendelea na zoezi la kutoa elimu ya kuweka madini joto katika bidhaa hiyo, ili kuwaondolea dhana potofu ati kuweka madini joto katika chumvi kunapunguza nguvu za kiume kwa wanaume jambo ambalo halina mashiko kwa ustawi wa jamii’.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.