SIKU YA KWANZA
Wetland International ni Shirika lisilo la kiserikali linalo jishughulisha na kulinda na kuhifadhi maeneo oevu, limekutana na wadau wake mbalimbali wakiwemo viongozi na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya kibiti kujadili namna ya kuhifadhi miti ya mikoko isipotee katika ukanda wa delta ya rufiji Wilayani Kibiti.
Mkutano huo uliodumu kwa siku mbili umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Kibiti ukiwahusisha wadau mbalimbali ikiwa ni Pamoja na wananchi wanaoishi delta ya Kiongoroni na Salale kwa lengo la kukusanya maoni Ili kutambua namna ya kuhifadhi mikoko isitoweke.
“Tuko hapa kujadili na kuangalia jinsi gani tunaweza kushirikiana na jamii kulinda na kuhifadhi mikoko ili tuweze kunufaika na mikoko yetu”alisema Happy.
Katika Mkutano huo mtafiti mwandamizi wa misitu na uvuvi Happy Peter amesema kati ya aina 7 za mikoko zinazopatikana Duniani, aina 6 hupatikana delta ya Rufiji katika Wilaya ya Kibiti.
Pia Bi. Happy amesema katika maeneo ya ardhi oevu faida ya uwepo wa mikoko hususani katika delta ya mto Rufiji ni Pamoja na kuweza kutengeneza mazalia ya samaki, kupunguza ukali wa mawimbi, kuzuia taka Kwenda baharini nk. Vilevile Happy amesema mbali na faida pia kuna changamoto ambazo hujitokeza katika maeneo ya ardhi oevu kama vile mabadiliko ya tabianchi, uchafu wa taka zilizo kithiri mfano chupa na mifuko ya plastiki jambo ambalo hupunguza ukubwa wa eneo la mikoko.
Aidha Mtafiti na mtaalamu elekezi Dr. Emanuel Japhet amesema shughuli za kibinadamu zinachangia kuathiri zaidi kwa asilimia kubwa ukanda wa delta, akiongea kwa msisitizo Dr. Emmanuel amesema “ni bora kuhifadhi mikoko iliyopo kuliko kuanza kupanda upya kwani gharama za upandaji ni kubwa sana”. Pia akasema mikoko ya kupandwa na binadamu ni rahisi kupotea ukilinganisha na miti ya mikoko iliyoota kiasili hivyo Kuna kila sababu ya kutunza mikoko tuliyonayo na kuhakikisha haipotei.
Nae mratibu mfawidhi wetlands Tanzania Dr. Fredric Mngube amesema, Kuna kila sababu ya kuhakikisha mikoko inalindwa na haikatwi kwani miti hiyo inaweza kupotea kwasababu ukanda wa delta kuna jamii inayoishi na kufanya shughuli za kibinadamu. Mngube ameitaka jamii inayoishi maeneo ya delta kuacha tabia ya kuweka Kambi au viringe katika misitu ya mikoko, ikiwa ni Pamoja na maharamia wanao tumia mashine kukata miti hiyo.
Hata hivyo Afisa kilimo Wilaya ya Kibiti Ndg. Ismail Bainga amependekezanjia mbadala ya kusaidia jamii kuwa na shughuli za kibinadamu za kupata kipato Kwa njia nyingine na si Kwa kuharibu mikoko kama vile kupanda chikichi, korosho za muda mfupi, ufugaji wa kuku na kuanzisha uchimbaji wa mabwawa ya Samaki ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuepukana na ukataji wa miti ya mikoko.
Katika Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la Wetlands uliwahusisha viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya, wataalam, wawakilishi wa kulima na wafugaji kutoka maeneo ya delta.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.