TAREHE 14-7/03/2023 Madiwani Pamoja na wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ramadhan Mpendu wamefanya ziara ya siku 3 kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.
lengo la ziara hiyo ni kujifunza zaidi kuhusu kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji na namna Halmashauri ya Mbarali inavyoweza kukusanya mapato kupitia zao hilo.
Katika ziara hiyo madiwani na wakuu wa idara walipata nafasi ya kutembelea mashamba ya Kapunga Rice Estate yaliyopo kata ya Itamboleo ambapo waliweza kuona mashamba ya mpunga ya wakulima wadogo wadogo na ya wawekezaji. Pia wameona mashine za kukoboa mpunga na magala mbalimbali ya kuhifadhi mpunga au mchele. Vilevile Madiwani na Wataalamu wametembelea Banio la maji maarufu kama Inteki ya mchina iliyopo kata ya Lugelele linalotumika kuruhusu au kuzuia maji kuelekea mashambani.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti inatoa shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanal Denice Mwila, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Chuki Mbwanjine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ndg. Missana Kwangura, Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri hususani Mkuu wa idara ya kilimo Dr. Anania Sangwa na Afisa kilimo Yobu Mlomo, wawekezaji na wengine wote kwa ukarimu, mapokezi mazuri na huduma zote katika kufanikisha ziara hii.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.